ANZA KUTENGENEZA MAHUSIANO BORA KWA WATOTO WAKO WAKIWA CHINI YA MIAKA 4!
KAMA ni mmoja wa baba wa familia unayeishi pamoja na watoto wako, basi hii makala ni kitu kimoja cha muhimu kuweza kukisoma ili kuendeleza kukuza ustawi mzuri kati yako na watoto. Pia kama ni Baba ambaye kwa namna moja au nyingine haupo pamoja na watoto zako kwa muda huu, basi ni changamoto ambayo hauna budi kupambana nayo na kuweza kuishinda kwa kurudusha mahusiano hayo kati yako na watoto hususani wakiwa na umri usiozidi miaka 4.
WATOTO ni wa nani? Katika kujibu swali hilo, fikiria na fikra potovu iliyosambaa kwenye jamii zetu za ki Afrika ya kwamba watoto ni wa Mama! Kama bado upo kwenye karne ya 21 na ukawa na fikra hizo basi utazidi kutengeneza tabaka la mahusiano (Bond) yenye nguvu baina yako na watoto ukiwa Baba. Mzazi ni Mama na Baba, kwa nini ujitenge? Kunaweza kukawa na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wangu, ila kama unaishi na mwenza wako pamoja na mkafanikiwa kupata mtoto/watoto basi baba unatakiwa uwe mzazi tosha kwenye nafasi yako ukiwa nyumbani.
KWA NINI IWE MIAKA 0-4? Kuna usemi wa swahili unasema "Samaki mkunje angali mbichi", katika kizazi hichi cha kidigitali, makuzi ya watoto huwai mapema sana, uelewa wa haraka na utambuzi wa awali umekua mapema sana kulinganisha na vizazi vingine vilivyopita. Kwa tafiti kadha za kisayansi na maadali ya jamii zinaonyesha mtoto anatengeneza mahusiano yenye nguvu (Bond) na mzazi kuanzia miaka 0-4 kwa njia kuu ya malezi na upendo. kuna athari kubwa sana kama Baba mzazi usipokua makini kwenye umri huo, kwani ni rahisi pia watoto kurithishwa Baba mwingine uku ukiwa hai.
KATIKA malezi ya awali na upendo, hapo ndipo unatengeneza mfumo thabiti wa makuzi bora na utambuzi wa awali kama baba tosha kwa mtoto. Katika mfano wa kidigitali tunaweza kusema unatengeneza software na kuiweka kwenye hardware ili iweze kufanya kazi. Wa Baba wengi wamekua wakiacha mama aingize software ambapo kwa asilimia 70 inakuweka kando Baba hapo baadae mtoto akishakomaa kiakili. Inawezekana pia mama akatengeneza mfumo bora bila ya kuathiri mahusiano kati yako na watoto ila yale matendo kwa njia ya malezi na upendo yana athari ya moja kwa moja. Kwa nini Baba usianze mapema?
MUDA bado upo, kwenye nyakati hizi za kidigitali ambapo wa mama wapo na shughuli nyingi sana za kiuchumi (kazi, biashara, bikoba n.k), Baba ni muda wa kuibuka shujaa! Sisemi kua mama hatahusika lakini inaweza kuwa 50/50 kwenye malezi na kutengeneza matokeo bora kwa watoto kwa njia ya malezi. Ukiwa unafanya kazi, umeajiriwa au umejiajiri usikubali kuwa busy kiasi cha kutoweza kufatilia kwa karibu shughuli za malezi kwa watoto na muda wa kuonyesha upendo. Kama unaishi pamoja nao basi unanafasi kubwa sana na haina sababu ya kufeli kipengele hichi muhimu.
MALEZI na upendo kwa mtoto ni pamoja na shughuli zinazoambatana na hatua za makuzi ya mtoto toka yupo tumboni kwa mama mzazi mwenza. Kwa mfano; Kufika kliniki kabla na baada ya mama kujifungua, kumpeleka mtoto kliniki kwa ajili ya kufahamu maendeleo ya afya, kumbembeleza wakati wa kulala au kula, kucheza nae wakati wote mkiwa wote, kumfundisha na kumpigia hadithi, kumbeba mgongoni au shingoni nakutembea nae, kumlisha chakula, kumsaidia kazi za shule, kumuogesha na kumvalisha n.k!
NAWEZA kukuhakikishia ya kuwa, hakuna furaha na faraja inayoweza kufikia ile ya kuonyesha upendo na watoto wakiuhisi upendo wako katika malezi kama baba mzazi. Nchi zilizoendelea zimeonekana kuweka mikakati mikubwa na endelevu ya kujenga asili ya baba kua mlezi bora kwa watoto, na hii imetokana na tafiti mbali mbali walizofanya na kuona matokeo bora yatatokana na BABA kuwa zaidi ya kiongozi wa familia ila kwenda hatua mbele zaidi katika malezi. Ukiangalia sinema, katuni na tamthilia utaweza elewa jinsi gani baba anavyowekewa uhusika katika familia, BABA ni kitivo cha malezi na upendo katika familia na ivyo ndivo inavopaswa kua katika karne hii ya 21.
NANI anaweza kutambua umuhimu wa kutengeneza Bond na watoto wako ingali mapema zaidi yako? Kasumba ya kuwa baba bora inayofananishwa na kuwa mme bwege/ baba dhaifu n.k au kuonekana tofauti katika jamii, inatakiwa ikanushwe na ikemewe kufika mwisho kwa mafanikio ya malezi bora kwa watoto wetu. Basi kuna baadhi ya SIRI ambazo nkina mama labda hawawezi kukueleza kuhusu watoto, mengine wanaweza kukwambia ila ningependa kukupa dondoo chache kuhusu tabia moja kubwa ya watoto hususani kuanzia miaka 0-2, na hii sio nyingine bali ni KULIA.
WATOTO wanapenda kulia, lakini sio kweli kulia ni dalili ya kuchukizwa au kutopendezwa na wewe ukiwa kama baba mzazi. Utasikia "unaweza kukaa na mtoto kweli?, akilia utaweza kumpa nyonyo?" na hii kauli inawafanya wa Baba wengi kuogopa kabisa mambo ya malezi na kuwaachia nafasi hii adhimu nkina mama tu. Sasa ni hivi, mtoto akilia ni kwa sababu tu hawezi kuongea maana bado yupo kwenye hatua ya kujifunza. Mtoto akilia anatoa tu ishara ya kitu fulani ambacho kinaendelea katika mwili wake. Ukishajua vizuri mbinu hizi hutoogopa tena mama akikuachia mtoto siku za mapumziko kwa sababu anaenda vikoba (Utani)!
KULIA inaweza kutokana na njaa, basi unaweza kumpatika maziwa, uji, juice kama ameshaota meno unaweza mpatika viazi, wali n.k. Mtoto anaweza kulia sababu ya usingizi, hapo kazi ni kumbembeleza kwa kumbeba mgongoni au kwenye mikono mpaka atapoweza kulala. Pia anaweza kulia sababu ya kutaka kumbadilisha nguo, labda anahisi uchafu kama umemvalisha pampasi na imeshajaa kwa muda mrefu au hajaoga kwa siku anaweza kulia kwa kuhitaji kusafishwa pia. Endapo mtoto atalia kwa muda mrefu na ivyo vyote umeviweka sawa basi atakua anahisi maumivu au ugonjwa ivo inabidi umuone daktari. Nafikiri nimeweza kukupa maarifa na mbinu ya kuepukana na adha hii ya kulia kwa mtoto.
MAMBO ni mengi na yana msingi pekee kwa Baba kudumisha malezi na upendo kwa watoto angali wakiwa wadogo kati ya miaka 0-4, ila kwa leo ninaweza kuishia hapo japo nitazidi kutoa machapisho kadhaa kuhusu hii dhana bora ya kujenga uhusiano madhubuti (Bond) na watoto zetu. Hii ni karne ya mtego sana, mama wa watoto zetu asilimia kubwa wapo busy na shughuli za kutafuta fedha uku sie wa Baba pia tunakua busy sana tunaonyesha upendo na malezi kwa njia ya kugharimia huduma (njia isiyo na manufaa kwetu) na kuona tunafanya la maana sana kumbe sio. Watoto wanalelewa na wasaidizi wa kazi na inafika hatua kabila ya mtoto inakua ya mdada wa kazi kwa sababu ya uhusiano bora toka kwake kwa watoto. Kwani huajwai ona watoto wanampenda mdada kuliko baba na mama?
NISEME tu, Baba unakila sababu ya kuwa kitovu cha upendo, malezi na ujenzi wa mahusiano bora kwa watoto katika hatua ya awali kabisa kuanzia miaka 0-4, ili mfumo wa maisha(software) kwa watoto zetu uwe kama tunavoutarajia hapo baadae. Pia ata kama umechelewa kutengeneza mahusiano bora na muunganiko toka awali basi unaweza kuanza sasa, kwani waswahili wanasema "usipoziba ufa basi utajenge ukuta". Mtoto akikua nakuanza kujielewa zaidi kufika hatua ya kufanya maamuzi yake itakua rahisi sana kukuelewa Baba na kukutii, kukupenda, kukuheshimu na kukuthamini kama atavyofanya ivo pia kwa mama.
INAWEZEKANA unaweza ukawa na tukio la furaha au huzuni katika familia yako, ukawa unajiuliza ni nani anaweza kusaidia kufanikisha jambo ilo. Naweza kukupa msaada huo kwa kukuhakikishia huduma bora kabisa kutoka SKYFALL EVENTS & DECORATIONS wanaoshughulika na huduma za kupamba na kuratibu matukio ya birthdays, harusi, misiba, send offs n.k., unaweza kuwafatilia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii kwa kubofya hii link SKYFALL COLLECTIONS OFFICIAL
SIO KWELI, kwamba hakuna wasaidizi bora wa kazi za nyumbani. Inawezekana haujawahi kupata taarifa sahihi ya wapi unaweza kupata wasaidizi bora wa kazi za majumbani ( house maids, gardeners, babby sitters, nannies, house helps, drivers n.k) wanaoaminika na wachapa kazi. Naweza kukuhakikishia huduma bora kabisa wanatoa hawa PRECIOUS DAY WORKERS TANZANIA ambapo utapata suluhisho bora na kukupa kile kinachostahili kwa wakati sahihi, unaweza kuwafatilia kwenye mitandao yao ya kijamii kwa kubofya hii link PRECIOUS DAY WORKERS OFFICIAL PAGE
KWA KUMALIZIA napenda kukutoa hofu wewe Baba unayeona swala hili ni changamoto kubwa kwako, unajiuliza utaanzia wapi au umechelewa au hutoweza, nataka nikupe moyo kuwa hakuna jambo linaloshindikana ukiweka nia na lengo la kuweza kutimiza jambo lako. Ni rahisi sana kutengeneza kuliko kurekebisha usichotengeneza. Pongezi kwa wakina Baba wote tuanofanikisha kipengele hiki kwenye karne hii ya 21 hakika tunanafasi yetu katika mioyo ya watoto zetu na ata kwa baba aliye juu mbinguni.
Imeandaliwa na Mr. Peter John | Dribble Da Mania.
Kwa mawasiliao, whatsapp: +255 759 850 259
Comments
Post a Comment